KAMAZI
Event Image

KUHUSU JUKWAA HILI

Kamazi Charity Fund tunaungana na mashirika mbalimbali duniani ya asasi za kiraia kama vile
makampuni ya kijeshi,team za michezo,sekta ya elimu,makampuni ya kibiashara, mashirika ya
afya,mashirika ya dini na wadau wote wenye uzalendo wa kusaidia jamii!
Mpango kazi uliopo mbele yetu mwaka 2026 ni Ujenzi wa kituo maalumu cha kuhudumia watoto
kwenye ukanda wa kusini magharibi mwa Tanzania ambapo ni eneo lenye raia wengi wenye
kuhitaji huduma zetu!
Aidha kwa ushirikiano mkubwa tulionao na kanisa la Russian orthodox Tanzania tunawakaribisha
waumini wote wa ki Kristo kusoma makala mbalimbali kuhusu kanisa hili la kiothodox nchini
Tanzania linaloendesha mission zake mbalimbali za kulitangaza neno la Mungu barani Afrika.
Bila kubagua imani ya mtu nivyema wote tukashirikiana kwasababu tumeumbwa na Mungu mmoja
wa mbinguni, je tunawezaje kuufikia ufalme wa baba Mungu wetu bila kusaidia ndugu zetu?
Kwa hakika hilo haliwezekani hivyo tuujenge undugu, upendo,amani na mshikamano.
Mpendwa msomaji ipo mifano hai ya machafuko na ukosefu wa amani katika baadhi ya mataifa
ndani ya Afrika kama vile Kongo DRC,Somalia,Sudani kusini,Libya,Mali nakwingineko ambapo
watu hao uishi maisha ya shida sana kukosa chakula, Maji pamoja na mahitaji muhuni ya
kibinadamu.
Tunawaomba sana wasomaji wetu kutembelea tovuti hii mara nyingi zaidi ili kwa pamoja tuweze
kuwanusuru wenzetu wanaokabiliwa na baa la njaa, vita,ukame na mafuriko,hakika tutauona
ufalme wa mbinguni.

Photo Library & Past Events