Ni shirika lisilo la kiserikali lilianzishwa mwaka 2025 na mwanaharakati wa asasi za kiraia,lengo kuu ikiwa ni kusaidia watoto masikini wa kiafrika na watu wasiojiweza kifikra,kiuzalendo,kiuchumi na kisiasa!
Shughuli kubwa hasa ndani ya KCF ni kupokea na kutoa misaada ya aina yoyote ya kibinadamu
kwa walengwa katika bara la Africa hasa nchi za ukanda wa mashariki zinazogubikwa na wimbi
kubwa la umasikini na njaa.
Mwanaharakati mwandamizi wa KCF analenga kufika mbali zaidi kwa kuibua vipaji mbalimbali vya
watoto wanaoishi mazingira magumu kulingana na vipawa walivyopewa na Mungu aidha kutoa
elimu ya kijamii kama vile fikra chanya za kimaendelo na uchumi kwa ujumla.
Katika jamii mbalimbali zilizoathirika na majanga ya vita,umasikini wa kupindukia,madawa ya
kulevya na waathirika wa HIV ADS nivyema watu hawa wakapewa msaada stahiki ili wajiskie
wenye amani ya kuishi kama watu wengine.
Hivyo basi KCF tunaungana na marafiki duniani kote ili tuweze kufikia malengo chanya ya
kumkomboa mwafrika ambaye mpaka karne hii bado hajaweza kujitegemea mwenyewe kupata
mahitaji ya msingi ya kibinadamu.
#Kwa pamoja tunaweza
KUMBUKA KUWA KCF inatoa huduma za usaidizi wa afya ya akili na kisaikolojia kwa watu binafsi na jamii katika nchi kadha wa kadha zilizoathiriwa na migogoro. Huduma hizi zimeunganishwa katika mipango ya kujenga amani. Kwa kuwasaidia watu kujenga upya uaminifu baina ya watu na jumuiya na kuwasaidia kurekebisha uhusiano uliofifia ndani ya jamii, afya ya akili na usaidizi wa kisaikolojia hushughulikia misingi ya ustawi wa mtu binafsi na kijamii. Kwa upande mwingine, inachangia kutatua vurugu na kujenga jumuiya zenye nguvu zaidi zinazoweza kupinga migawanyiko, mishtuko na mizozo. Kuanzia Tanzania hadi Burundi,Kongo,Malawi na Sudani kusini, hatua za afya ya akili na usaidizi wa kisaikolojia za KCF zitasaidia maelfu ya watu kama kurekebisha uhusiano, kurejesha hali ya ustawi ndani ya familia kwa ujumla kwenye jamii zao. Miradi ya usaidizi wa afya ya akili na kisaikolojia wa KCF ni pamoja na kusaidia wanaorejea katika kujenga upya maisha yao, kuwafunza kuwa wapatanishi katika ujuzi wa kutatua migogoro, kuwasaidia walinda amani na kuhudumia vyema watu wengine.